Kazi mpya ya rapper na mtangazaji wa East Africa Radio, JR Junir akimshirikisha Nay wa Mitego. Inaitwa Mapichapicha na imetayarishwa na Mona Gangster.
Home » September 2016
Thursday, September 29, 2016
Tecno wazindua Phantom 6 na Phantom 6 Plus zinazoleta mapinduzi ya teknolojia
Kampuni inayoongoza kwa mauzo ya simu Afrika, Tecno Mobile imezindua simu mbili matata za Phantom 6 na Phantom 6 Plus katika tukio lililohudhuriwa na watu maarufu kibao katika hoteli ya Armani ambayo ipo katika jengo refu zaidi duniani Burj Khalifa.
Uzinduzi huu umefanyika wakati ambapo kampuni ya Tecno inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.
ANGALIA KIPANDE KIFUPI CHA VIDEO YA TECNO PHANTOM 6
Uzinduzi huu umefanyika wakati ambapo kampuni ya Tecno inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.
ANGALIA KIPANDE KIFUPI CHA VIDEO YA TECNO PHANTOM 6
“Imetuchukua takribani miaka 3 katika matengenezo yake na imehusisha zaidi ya wahandisi laki 5,” alisema Mkuu wa Masoko wa Tecno, Vane Ni.
“TECNO Phantom 6 inawapa watumiaji wa simu za mkononi utulivu bora pindi wanapotumia, kasi na kamera bora na nzuri ili kufurahia zaidi simu ya mkononi,” alisema Naibu Kiongozi wa Masoko wa Tecno Nigeria, Attai Oguche.
Uzinduzi ulifana sana ambapo kulikuwa na zaidi ya vyombo vya habari 70 tofauti kutoka nchi mbalimbali duniani kote na miongoni mwa mastaa waliohudhuria ni mwanamuziki mahiri wa Tanzania, Alikiba na mwanahabari ‘Mtuwa Nguvu’ Millard Ayo ambaye alishinda safari ya kwenda China.
Mwanamuziki wa kimataifa wa Tanzania, Alikiba akiwa na kifaa kipya cha Phantom 6 akifanya mauzungumzo
Baada ya uzinduzi huo Tecno Tanzania ikatangaza kwamba Phantom 6 na Phantom 6+ zitaanza kupatikana rasmi kuanzia tarehe 8 Oktoba 2016 katika duka la Tecno lililopo City Mall Posta ambapo wateja wote watakaonunua Phantom 6 siku hiyo watapatiwa vifurushi vya zawadi na kutakuwa na zawadi kubwa nono.
Pia wakatangaza kwamba kuanzia Jumatatu tarehe 3 Oktoba wateja watajaza fomu maalum ili kuweka oda zao na watazawadiwa zawadi mbalimbali zikiwemo T-Shirts, mabegi, T-Band na Sefie stick siku ya kuanza mauzo hiyo tarehe 8 Oktoba.
Kuhusu bei kwakweli Tecno wameangalia hali halisi ya uchumi kwa sasa ambapo gharama itakuwa kati ya Tsh 500,000 – Tsh 600,000.
Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno nahakikisha hukosi moja wapo ya simuhizi kali ambazo zimekuja kufanya mageuzi ya teknolojia.
Diva: Mastaa wa Bongo waelewe thamani yao, mimi nachaji milioni 3.5 kwa appearance tu
Mtangazaji wa Clouds FM, Diva The Bawse amewataka mastaa wa Tanzania kutambua thamani ya brand zao na kuacha kujichukulia poa.
Amedai kuwa mastaa wengi wamekuwa wakitumika bure kufaidisha watu wengine na anadhani ni muhimu wakaacha kujishusha kiasi hicho.
Anadai kwa upande wake yeye, hafanyi kitu bure na kudai kuwa hata kuonekana kwenye saa moja kwenye party ya mtu, ni lazima awe amemlipa.
“My standard rate is 3.5 million in one night that including 30 minutes hosting, na sikai less than hour naondoka,” Diva ameandika kwenye blog yake.
“Ifike stage celebs wajue value yao na sio kutumika tu kwa faida ya watu wengine. Chochote unaona pia napost kwenye account zangu za mitandao kinalipiwa., lazima ujue kama wewe ni maarufu lazima ulipwe hata kutweet brand ya mtu mwingine,” ameongeza.
Mtangazaji huyo ana zaidi ya followers milioni 1.1 kwenye Instagram na amekuwa akiingiza mkwanja mrefu kwa kupost matangazo mbalimbali
Nas B ft Baridi Band – Tunatumia VIDEO
Msanii wa muziki, Nas B ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Tunatumia’ akiwa amemshirikisha Baridi Band. Video imeandaliwa na director, Jukya.
Kevin Hart aongoza orodha ya wachekeshaji wanaolipwa zaidi duniani
Forbes wametoa orodha mpya ya wachekeshaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani. Kevin Hart ndiye anayeongoza orodha hiyo akiwa amelipwa kiasi cha $87.5 milioni kuanzia mwezi Juni mwaka mpaka kufikia Juni mwaka huu.
Nafasi hiyo kwa muda mrefu imekuwa ishikiliwa na Jerry Seinfeld ambaye kwa sasa ametupwa kwenye nafasi ya pili. Kwenye orodha hiyo pia yupo mchekeshaji wa kike, Amy Schumer.
Hii ni orodha ya wachekeshaji wengine wanaolipwa zaidi.
1) Kevin Hart ($87.5 million)
2) Jerry Seinfeld ($43.5 million)
3) Terry Fator ($21 million)
4) Amy Schumer ($17 million)
5) Jeff Dunham ($13.5 million)
6) Dave Chappelle ($13 million)
7) Jim Gaffigan ($12.5 million)
8) Gabriel Iglesias ($9.5 million)
9) Russell Peters ($9 million)
10) John Bishop ($7 million)
2) Jerry Seinfeld ($43.5 million)
3) Terry Fator ($21 million)
4) Amy Schumer ($17 million)
5) Jeff Dunham ($13.5 million)
6) Dave Chappelle ($13 million)
7) Jim Gaffigan ($12.5 million)
8) Gabriel Iglesias ($9.5 million)
9) Russell Peters ($9 million)
10) John Bishop ($7 million)
Donald Trump akasirishwa na wasaidizi wake kukiri kuwa alibwagwa na Clinton kwenye mdahalo wa kwanza
Donald Trump anaamini kuwa alifanya vizuri kwenye mdahalo wa kwanza dhidi ya Hillary Clinton – lakini kura zinasema tofauti, hata wasaidizi wake pia wanaamini kuwa alikula za uso!
Kinampa hasira kuona kuwa wasaidizi na washauri wake wanakubali maneno ya vyombo vya habari kuwa hakufanya vyema kwenye mdahalo huo, kwa mujibu wa CNN.
Wasaidizi wake walimshauri abadilishe namna anavyojiandaa kwenye mdahalo ujao lakini hataki kusikia lolote.
Trump anataka wafuasi wake wamtetee kwa anachokifanya na amekataa kukubali kuwa alifanya vibaya licha ya kura kuonesha kuwa Clinton alipata asilimia zaidi ya 60 huku yeye akicheza kwenye 27 tu.
Wagombea hao wa Urais wa Marekani watakutana kwenye mdahalo wa pili October 9.
Nuh Mziwanda azinguana na uongozi wake, adai viongozi wanataka umaarufu kuliko kazi
Mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda amezinguana na uongozi wake ambao alikuwa anafanya nao kazi kwa madai umeshindwa kufanya kazi aliyoitaka
Mapema mwaka huu Petit Man alimchukua msanii huyo na kuamua kumsimamia ikiwa ni wiki chache toka aachane na wasanii wa Endless Fame ya Wema Sepetu.
Mapema mwaka huu Petit Man alimchukua msanii huyo na kuamua kumsimamia ikiwa ni wiki chache toka aachane na wasanii wa Endless Fame ya Wema Sepetu.
Nuh amedai yeye ni msanii mkubwa na meneja huyo ameshindwa kumfikisha pale ambapo alikuwa anataka kwenda.
“Nimetoka kule kwa ajili tu ya sababu zangu binafsi inabidi ni’move on, mi sio msanii mdogo inabidi niwe na meneja ambaye anajielewa na anajua msanii ambaye ninaye ni msanii ambaye yupo katika level gani, kama meneja anashindwa kujua msanii ambaye anafanya naye kazi siwezi kudeal naye, kwa sababu nilishapotezaga time katika muziki three years kwenye mapenzi, sa siwezi kupoteza mwezi mmoja kwa mtu ambaye kanikuta tu nimeamua kufanya naye kazi, kwa hiyo ni bullshit mi naachana naye naendelea na mambo yangu mengine”, Nuh Mziwanda alikiambia kipindi cha Planet bongo cha EA Radio.
Aliongeza, “Siyo kwa ubaya kwa uzuri, niliamua kufanya naye kazi, lakini kashindwa kupresent kile kitu ambacho mi nilikihitaji, narudia tena mi ni msanii mkubwa, inabidi ajue msanii mkubwa inabidi awe na nini na nini, kuna vitu avijue kama meneja, sasa kufanya kazi na meneja ambaye na yeye anataka ustar, ni kitu ambacho hakiwezekani”, alisema Nuh Mziwanda.
Nuh Mziwanda pia alisema anaamini jitihada zake ndizo zimemfikisha hapo alipo, na kukanusha kauli ambayo watu wengi wamesema kuwa kwa kuwa sasa ana studio, amekuwa na dharau kwa uongozi wake.
Tuesday, September 20, 2016
Sina mpango wa kutoa album Asema Dully Sykes
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amesema hafikirii kutoa album kabisa kwa siku za usoni kwasababu anaamini hazina faida kama zamani.
Akiongea na Planet Bongo ya EATV Dully alisema album zilikuwa zinaingiza pesa kipindi kile yeye anaanza kufanya muziki.
“Album zilikuwa zina dili kipindi kile mimi naanza muziki, lakini siku hizi ujanja ujanja umekuwa mwingi sana. Siwezi kutoa album labda mpaka nisikie mapirate wameweza kudhibitiwa kikamilifu,” alisema.
Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake, Inde aliomshirikisha Harmomize
Brown Mauzo Ft Alikiba – Nitulize
Msanii Brown Mauzo kutoka nchini Kenya ameachia wimbo mpya unaitwa “Nitulize” amemshirikisha King kutoka Tanzania Alikiba, Studio Combination Sound.
Serengeti Boys kuweka kambi nje nchi
Baada ya kuifunga Congo-Brazzaville mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika, timu ya taifa ya vijana, Serengeti inatarajiwa kuondoka Alhamis wiki hii kwenda kupiga kambi nje ya nchi.
Hata hivyo, taratibu zinapangwa kuhakikisha kwamba timu hiyo inakwenda kupiga kambi kwenye nchi tulivu inayolingana hali ya hewa na Congo Brazzaville kadhalika chakula pamoja na mazingira.
Tanzania na Congo Brazzavile, zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2, 2016 huko Congo Brazzaville na timu itakayopata ushindi wa jumla katika michezo miwili itafuzu kwa fainali hizo.
Katika mchezo uliofanyika Septemba 18, Serengeti Boys ilipata mabao yake kupitia Yohana Mkomola na Abdi Makamba wakati yale ya Congo yalifungwa na Langa-Lesse Percy na Makouana Beni ambao mashabiki wa soka walikuwa wakiwalalamikia kuwa ni “wakubwa.”
Ili ifuzu kwa fainali zitakazofanyika mwakani huko Antananarivo, Madagascar katika fainali zitakazoanzia Aprili, 2017, Serengeti Boys inatakiwa ibaki na matokeo yake ya sasa na ihakikishe inapata ushindi na kama sare basi wapate bao kufuta faida ya bao la ugenini ambalo Congo Brazzaville walikuwa wanasheherekea baada ya mchezo.
Monday, September 19, 2016
Pogba awapa moyo mashabiki wake wa Manchester United
Mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa Paul Pogba wa Manchester United amelazimika kuwapa moyo mashabiki wake baada ya timu yake kupoteza mechi mbili mfululizo
Jumapili, Septemba 18 ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa tano wa ligi kuu ya England dhidi ya Watford na kufungwa magoli 3-1. Kiungo huyo wa Ufaransa ambaye hadi kwa sasa hajafanya vizuri kama wengi walivyokuwa wana matarajio akiwa na Man United toka avunje rekodi ya usajili.
Kupitia Instagram, Pogba ameandika: Asante kwa mashabiki wote kuwa pamoja na sisi matokeo bado sio mazuri kwa upande wetu, lakini tunaendelea kupambana, Man United tunaweza.”
Jux asema hapendi kuona msanii anajichukulia poa kwenye mwonekano
Msanii wa muziki Jux amesema mwonekano mzuri kwa msanii ni kitu muhimu ambacho kinamjenga msanii kujiamini pamoja na kuwa tofauti na wale anaowapa huduma
Akiongea na Clouds TV wiki hii, Jux amesema hapendi kuona msanii anashindwa kujali mwonekano wake.
“Sometime hata mimi mwenyewe sipendi kuona mtu au msanii kila siku yupo vile vile,” alisema Jux. “Kama msanii lazima ubadilike, hata mimi huwaga nikipost picha najiangalia naona hapa natakiwa kubadilika, hivi nimeshazoeleka,”
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na brand yake ya ‘African Boy’, amewataka wasanii wenzake kuhakikisha wanajiweka vizuri katika mwonekano.
Bushoke - Ushauri wa mashabiki hunijenga sana
Bushoke amedai kuwa ushauri kutoka kwa mashabiki hasa ule anaoupata kwenye mitandao ya kijamii humjenga.
Hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya uitwao ‘Mpita Njia’ ambao anadai kuwa mashabiki wengi wamempongeza. Akiongea na Bongo5 Bushoke amesema huwa anapenda kusoma sana koment za mashabiki wake na kuwajibu
“Unajua mimi huwa anapenda sana kusoma comment nione mashabiki wangu wanasema nini na wanatoa ushauri gani,” amesema. “Mimi huwa siogopi kusoma comment zaidi huwa napenda kuwaelewesha nikiona mtu ameuliza kitu ambacho anahitaji kueleweshwa huwa nafanya hivyo ili apate uhakika maana unajua mwingine anatamani kuonana na wewe lakini anakuwa hawezi, basi huwa nafanya hivyo kwa kuwajibu na kuwashukuru na kufanyia kazi mawazo yale ambayo naona ya muhimu,” ameongeza.
“Kuna wengine huwa wanazingua, hao huwa hawakosekani unajua ukishakuwa msanii lazima ukutane na vitu kama hivyo hasa katika mitandao. Wapo watakaokutia moyo na watakaokuvunja moyo, hizo ni changamoto tu.”
Hizi ni baadhi ya comments ambazo Bushoke alikuwa akiwajibu mashabiki wake na kuwaelewesha
Lulu adai sasa anahitaji kupata mtoto
Msanii mahiri wa filamu Bongo, Elizabeth ‘Lulu ‘ Michael amedai kuwa anahitaji mtoto kwa sasa.
Muigizaji huyo ameandika ujumbe kwenye mtandao wake wa Instagram akimuomba Mungu huku akidai kuwa yupo tayari kwa sasa na anahitaji mtoto.
“Okay…I’m ready noooowand I want a Baby BoyIn Jesus Name,” ameandika Lulu kwenye mtandao huo.
Kwa sasa muigizaji huyo yupo kwenye mahusiano na bosi wa EFM, Majay
Idris Sultan kuwania nafasi ya kuhost tuzo za MTV MAMA 2016
Mshindi wa shindano la Big Brother 2014, Idris Sultan ameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwa mmoja kati ya wachekeshaji watakao host kwenye tuzo za MTV MAMA 2016.
Kupitia mtandao wa Instagram wa MTV wameandika, “Would you nominate@idrissultan to HOST @mtvmamas on 22.10.16 #mtvmama2016 NAY or YAY.”
Wasanii wengine wanaowania nafasi hiyo ni pamoja na Basket Mouth (Nigeria), Idris Elba (Uingereza) na Kelvin Hart (Marekani).
Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Jumamosi ya Oktoba 22 kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome, Afrika Kusini.
Tuesday, September 6, 2016
Lil Wayne Aitukana Lebo Yake Ya Cash Money Kwenye Shoo!
Lil Wayne ameonesha kuwa bado anaichukia lebo yake ya Cash Money baada ya kuitukana wakati alipokuwa jukwaani kwenye ziara ya Drake ya Summer Sixteen huko Houston, Marekani
“I love y’all, I just want to say I love every single one of you, before noting how he’s been coming to that city since he was 14-years-old,” ameongea Wayne kwenye tamasha hilo. “But he didn’t stop there. So before I leave — I leave you with some kind words. F*** Cash Money!.”
Lil Wayne amekuwa na bifu na Birdman tangu mwaka jana huku rapper huyo akitaka lebo yake ya Cash Money kumlipa kiasi cha dola milioni 51 kwa kuchelewesha kuachia albamu yake iliyotakiwa kutoka mwaka 2014.
Fella Akwama: Juma Nature Hanitaki Anaona Sina Maana’
Mkurugenzi wa Yamoto Band na TMK Wanaume Family, Mkubwa Fella ameonekana kugonga mwamba juhudi zake za kutaka kurudisha mahusiano yake ya kazi na msanii wake wa zamani wa Kundi la TMK Family, Juma Nature.
Hapo awali Juma Nature alikuwa msanii wa Kundi la TMK Wanaume Family la Mkubwa Fella lakini baadae aliondoka na kwenda kuanzisha Kundi lake la TMK Wanaume Halisi. Akiongea Ijumaa hii, Fella amedai wasanii ambao wanamthamini ni wale ambao yupo nao.
“Mimi ndo hanitaki, anaona mimi sina maana, lakini walioona mimi na maana ndo hawa ambao nipo nao mpaka sasa,” alijibu Fella baada ya kuulizwa kama ana mpango wowote na Juma Nature kwa sasa.Kauli hiyo inaonyesha meneja huyo ameonga mwamba juhudi zake za kutaka kumrudisha msanii huyo kundini baada ya
kuhaidi mara kadhaa kufanya hivyoJoh Makini na msanii wa Nigeria, Falz kuungana kwenye Coke Studio Africa msimu wa 4
Msanii wa Hip Hop Bongo, Joh Makini yupo nchini Nairobi, Kenya akiwa ni miongoni mwa wasanii wanne watakaoiwakilisha Tanzania kwenye kipindi cha Coke Studio Africa Season 4.
Huu ni msimu wa pili kwa rapper huyo wa Bongo kushiriki kwenye kipindi hicho. Kwa msimu wa tatu, Joh Makini aliungana na msanii wa Nigeria, Chidinma ambaye walitengeneza mchanganyiko uliowavutia mashabiki wa kipindi hicho kitu kilichopelekea mpaka wakafanya collabo ya wimbo wa ‘Perfect Combo’.
Huu ni msimu wa pili kwa rapper huyo wa Bongo kushiriki kwenye kipindi hicho. Kwa msimu wa tatu, Joh Makini aliungana na msanii wa Nigeria, Chidinma ambaye walitengeneza mchanganyiko uliowavutia mashabiki wa kipindi hicho kitu kilichopelekea mpaka wakafanya collabo ya wimbo wa ‘Perfect Combo’.
Kwa msimu huu Joh Makini ameungana na rapper wa Nigeria, Falz ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Chardonnay Music’ lakini ikiwa ni msimu wake wa kwanza kushiriki kwenye kipindi hicho.
Huu ni wimbo wa Falz, ‘Chardonnay Music’ ambao ameuachia wiki iliyopita.
Ben Pol Asisitiza Kuitoa Album Yake Mwaka Huu
Ben Pol amedai kuwa mpango wa kutoa album yake mwaka huu upo pale pale.
Ameiambia Bongo5 kuwa album hiyo imechelewa kutoka kwasababu yeye na uongozi wake wanatengeneza mkakati wa kuipromote na kuiuza ili iende mbali na kumfikia kila shabiki aliyenuiwa.
Hata hivyo muimbaji huyo wa ‘Moyo Mashine’ amedai kuwa lengo la kuitoa si kupata fedha bali ana sababu zingine kuu mbili.
“Moja ni kutengeneza ukamilifu wa mwanamuziki,” anasema Ben.
“Mimi si mtu wa magumashi, kama unataka ukamilifu wa kuitwa mwanamuziki au msanii uliyekamilika, lazima uwe na album,” ameongeza.
“Lakini pili, nataka baadaye biashara ya album ikirudi kuwa stable, ikija kuwa ni deal yaani, niweze kuwa katika watu ambao walithubutu kutoa album licha biashara kuwa bado si nzuri, Ben Pol alikuwepo, kwahiyo niingie kwenye wale wanaharakati waliothubutu kurudisha biashara ya album regardless ya situation ya mauzo ya kipindi hicho au situation ya biashara yenyewe kwa ujumla.”
“Kwahiyo watu wategemee album yangu mwishoni mwa mwaka huu mzigo utatoka.!
Mkhitaryan Hana Uhakika Kama Atacheza Derby
Kiungo wa Manchester United na timu ya Taifa ya Armenia Henrikh Mkhitaryan hana uhakika kama atacheza Manchester Derby baada kuumia katika mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Czech jumatano iliyopita.
Henrikh Mkhitaryan kupitia akaunt yake ya twitter alipost ujumbe huu
Not sure yet if I’ll bit fit for the derby, but I’m motivated as ever to put all energy to be in great shape asap!!
Site Users
Popular Posts
Topics
News
(108)
Artists
(83)
Local
(45)
Views
(41)
Music
(38)
International
(36)
Relationships
(34)
Universities
(28)
Sports
(25)
Sports Stars
(25)
Business
(14)
Life Style
(14)
Actors
(10)
OFFclass
(10)
Entrepreneur
(9)
Events
(9)
Health
(9)
Hustles
(9)
Who Hit A Lottery?
(7)
Fashion
(4)
High Schools
(4)
Movies/TV Series
(4)
Talent
(3)
Education
(1)
Tech
(1)
Archive
-
►
2017
(182)
- November 2017 (2)
- September 2017 (20)
- August 2017 (46)
- July 2017 (6)
- June 2017 (2)
- May 2017 (1)
- April 2017 (45)
- March 2017 (51)
- February 2017 (8)
- January 2017 (1)
-
▼
2016
(94)
- December 2016 (1)
- November 2016 (3)
- October 2016 (22)
- September 2016 (68)