Home » March 2017
Friday, March 31, 2017
Thursday, March 30, 2017
Tuesday, March 28, 2017
Sarafu Kubwa ya Dhahabu Yenye Dhamani $4m Yaibiwa Nchini Ujerumani
Sarafu kubwa iliyotengenezwa kwa dhahabu, ambayo ina picha ya Malkia Elizabeth wa Uingereza, ambayo inakadiriwa kuwa na thamani ya $4m (£3.2m), imeibiwa kutoka kwenye makumbusho Ujerumani.
Sarafu hiyo kutoka Canada imeandikwa kuwa ya thamani ya $1m, lakini kwa sababu imetengenezwa kwa kilo 100 za dhahabu, thamani yake ni ya juu sana kwa kutumia bei ya sasa ya dhahabu.
Emanuel Austin Kuendesha Semina ya Bure ya Dance Alhamis Hii Dar
Mwalimu wa dance mwenye mafanikio makubwa na mwenye shule maarufu inayofundisha fani hiyo nchini Ujerumani, Emanuel Austin anatarajia kufanya semina ya dance jijini Dar es Salaam Alhamis hii.
Hii ni taarifa rasmi kuhusu semina hiyo:
Harmo Rapa-“Mimi Binafsi Naweza Kumhudumia Wema Sepetu Kwenye Mapenzi”
Msanii wa Bongo Fleva, Harmo Rapa kwenye studio za millardayo.com alifunguka
na kueleza hisia zake za
kimapenzi kwa mastaa watano kutoka Tanzania.
Miongoni mwa
mastaa aliowataja ni pamoja na staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu na kuyaongea haya “Wema Sepetu ni mmoja kati ya wanawake wanao nivutia sana
hasa lile umbo lake matata na kummudu pia sishindwi ninaweza kumhudumia kwa
kila kitu hata kumnunulia nyumba na gari.” – Harmo Rapa.
Wanasayansi Mamegundua Mnyama Mwenye Ubongo sawa na Binadamu
Utafiti mpya uliyofanywa na Chuo Kikuu cha New York, Marekani umegundua mnyama mwingine ambaye ana
ubongo mkubwa sawa na binadamu ambapo utafiti huo ulionesha jinsi gani
mazingira wanayoishi binadamu na Nyani yanavyoshabihiana na kuwafanya kuwa
wanyama pekee wenye ubongo ulio sawa kwa ukubwa.
Mkuu wa utafiti huo Alex Decasian alizungumza
na BBC “Nyani hasa jamii ya Orangutans wana ubongo ulio sawa na binadamu
kwa kuwa hupitia changamoto zinazofanana, nyani mwenye umri mkubwa ana
ubongo mkubwa zaidi kuliko Nyani mtoto, hii inasadia katika ulinzi wa
jamii yao na kutatua matatizo kama ugomvi”
Utafiti huo pia ulionesha nyani
anayekula matunda ana ubongo mkubwa zaidi ukilinganisha na nyani anayekula
majani na mizizi ambapo Mwanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Oxfordamesema
ubongo mkubwa humtofautisha nyani na wanyama wengine katika uelewa wa mambo,
kuwa na huruma na kutambua majukumu yao.
Uwanja Shanghai Shenhua Ulivyowaka MOTO
Uwanja unaotumiwa na klabu ya soka tajiri katika ligi kuu ya China, Shanghai Shenhua ambao anachezea Carlos Tevez umeshika moto Jumanne hii.
Hata hivyo moto huo ulifanikiwa kuzimwa mapema japo chanzo cha moto huo hakijafahamika zaidi. Tazama zaidi picha za tukio hilo hapa chini.
Hata hivyo moto huo ulifanikiwa kuzimwa mapema japo chanzo cha moto huo hakijafahamika zaidi. Tazama zaidi picha za tukio hilo hapa chini.
Nick wa Pili afafanua Maana ya Wimbo wa ‘Ya Kulevya’
Leo March 28 2017 kupitia kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM wasanii wanaounda kundi la Weusi wamefunguka rasmi kuhusu maana halisi ya wimbo wao mpya wa ‘Ya
kulevya’ na kusema wimbo huu unamzungumzia baba wa familia kama kiongozi
aliyepewa dhamana ya kuiongoza familia na si kama wengine wanavyofikiria
tofauti.
“Inamzungumzia baba wa familia kama kiongozi
aliyepewa dhamana ya kuiongoza familia, mama na familia imempenda sana baba,
kawaida ya baba akipendwa anachukulia poa, upendo umemlevya baba anaanza
kufanya mambo yasiyofaa, anakuwa mtu wa ‘totoz’au Kiki”-Nikki wa Pili
”Msanii ni zao la mazingira yake tumetumia
maneno yanayozunguka sasa hivi tumeyatoa kwenye ‘muktadha’ yake tumeyaleta
kwenye wimbo wetu tukatoa kitu”:-Nikki wa Pili
Hata hivyo Weusi wamewaahidi mashabiki zao kuwa watawaletea Video mpya ya wimbo huo soon
Bill Nass Afunguka 'Why' Relationship Yake Haiweki Wazi
Je unajua sababu inayomfanya Bill Nass awe msiri katika mahusiano yake?
Rapper huyo amefunguka sababu inayomfanya awe hivyo. Akiongea na kipindi cha Bongo Dot Com cha Times FM, hitmaker huyo wa Mazoea amesema alishawahi kuwa katika mahusiano mengi ambayo ambayo hakuwa na bahati nayo.
“Nimekuwa kwenye mahusiano mengi ambayo sikuwa na bahati nayo pia inaweza kukutengeneza kisaikolojia kutokana na mambo ambayo nayaona kwa rafiki zangu. Nina bahati ya kuona hivyo vitu kwa hiyo sijui huko mbele mahusiano ni suala la feelings,” amesema rapper huyo.
Bill ameongeza kwa sasa hana mahusiao na mrembo yoyote wala hajawahi kufikiria kuoa hivi karibuni.
Nape Nnauye alivyokabidhi ofisi kwa Waziri Mwakyembe
Aliyekuwa Waziri wa
Habari, Sanaa, Utamadunu na michezo, Nape Nnauye leo amekabidhi ofisi kwa
Waziri Mpya wa Wizara hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe. Makabidhiano hayo
yamefanyika katika ofisi za Wizara Dodoma.
Aliyekuwa Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye leo amekabidhi rasmi ofisi
kwa Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Katika makabidhiano
hayo yaliyohudhuriwa na watendaji wakuu wa Wizara, Mhe. Mwakyembe ameahidi kuwa
licha ya kukabidhiwa ofisi, anaamini kuwa Mhe. Nnauye bado ni mdau mkubwa wa
sekta za Wizara na kuwa anategemea kuendelea kupata ushirikiano kutoka kwake.
Aidha Waziri Mwakyembe
ameahidi kuendeleza yote mazuri yaliyo anzishwa na Nnauye katika kuimarisha
ufanisi wa Wizara na kuhakikisha inakuwa ni moja ya Wizara za mifano nchini.
Amesisitiza kuwa katika kipindi kifupi alichokaa Wizarani, Mhe. Nnauye
alianzisha mabadiliko makubwa na watu wameanza kuifahamu vizuri Wizara.
Kwa upande wake Nnauye
amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumpa dhamana kubwa ya
kusimamia Wizara kwa kipindi cha miezi 15 huku akiwa ndio kwanza amekuwa mbunge
katika awamu yake ya kwanza. Aidha Nnauye ameahidi kuendela kushirikiana na
Wizara kwa ukaribu kwani ni kweli yeye ni mdau mkubwa wa sekta za wizara hii.
Nay wa Mitego Ajibu Kuhusu Kudaiwa Kutumika Kisiasa
Msanii kutoka Bongoflevani Nay wa Mitego amezidi kuzichukua headlines baada ya Serikali kutoa agizo la kuachiwa na Polisi alipokuwa anashikiliwa kutokana na wimbo wake wa ‘WAPO’ kudaiwa kuwa hauna maadili.
Baada ya kuachiwa na Polisi kituo cha TV cha Azam wamefanya interview na Nay wa Mitego na wamemuuliza mambo mbalimbali ikiwemo kudaiwa kutumika kisiaasa, Bonyeza play hapa chini kufahamu alichokijibu Nay wa Mitego
Weusi – Ya Kulevya
Weusi wameachia kazi mpya waliyoipa jina YA KULEVYA. Wimbo umetayarishwa na Buggahleez na mastering kufanywa na Chizan Brain.
Monday, March 27, 2017
Rais Magufuli Apandisha Cheo Maofisa wa Uhamiaji
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewapandisha cheo maofisa sita wa Uhamiaji kuwa makamishna wa Uhamiaji na kuwateua kushika nyadhifa mbalimbali katika Jeshi la Uhamiaji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, kupandishwa vyeo na uteuzi huo umeanza tangu Februari 28, mwaka huu.
Aliwataja walioteuliwa kushika nyadhifa hizo ni Mrakibu wa Uhamiaji (SI) Edward Chogero kuwa Kamishna wa Divisheni ya Fedha na Utawala, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Samwel Magweiga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Udhibiti na Uongozi wa Mipaka na Mrakibu Mwandamizi (SSI) wa Uhamiaji Gerald Kihinga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Pasipoti na Uraia.
Wengine ni Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Musanga Etimba kuwa Kamishna wa Divisheni ya Hati za Ukaazi na Pasi na Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Hannerole Manyanga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria.
Pia taarifa hiyo ilieleza kuwa Rais Magufuli amemteua Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Mourice Kitinusa kuwa Kamishna Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA)
Taifa Stars kuikaribisha Burundi kesho Uwanja wa Taifa
Taifa Stars, Jumanne hii jioni inaingia tena Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kucheza na Intamba Murugamba ya Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, kwa mujibu wa kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa ya FIFA.
Huu ni mchezo wa pili kwa Taifa Stars kucheza ndani ya wiki moja baada ya ule wa awali dhidi ya The Zebras ‘Pundamilia’ wa Botswana uliofanyika Uwanja huo wa Taifa, jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.
Katika mchezo huo wa Jumamosi, Taifa Stars ambayo kwa sasa inanolewa na Salum Mayanga akisaidiwa na Patrick Mwangata ambao ni makocha wapya wa kikosi hicho, walishinda kwa mabao 2-0.
Tayari Intamba Murugamba wametua nchini tangu jana Jumapili saa 4.30 asubuhi na kufikia Hoteli ya De Mag iliyoko, Kinondoni, Dar es Salaam na jioni yake walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini. Leo Jumatatu, inafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ndani ya kikosi hicho wamo washambuliaji wawili wanaotamba katika klabu za Simba na Young African za Dar es Salaam. Nyota hao ni Amisi Tambwe wa Young Africans na Laudit Mavugo wa Simba.
Leo Jumatatu Machi 27, 2017 saa 8.30 alasiri nyota hao wakiongozana na kocha wao watazungumza na wanahabari namna walivyoajiandaa kucheza na Taifa Stars ambayo pia ina nyota wengi wanaocheza na wachezaji hao wa Burundi katika klabu za Simba na Young Africans.
Wakati Mavugo ni mshambuluaji, anatarajiwa kuwa na wakati mgumu mbele ya walinzi mahiri ambao pia wako Simba kama vile Abdi Banda na Mohammed Hussein wakati Andrew Vicent anayetoka Young African atakuwa kisiki kwa Tambwe wanayecheza naye timu moja kama makocha watawapanga.
Kwa upande wake, Mayanga alifurahishwa na ushindi wa Jumamosi iliyopita dhidi ya The Zebras ya Botswana na hivyo amehimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa kesho.
Katika kuunga mkono wito wa Kocha Mayanga, TFF imebakiza viingilio vya mchezo huo kuwa sawa na vile vya Jumamosi iliyopita kwani katika mzunguko ambao unachukua mashabiki wengi kiingilio kitakuwa ni Sh 3,000.
Kwa upande wa VIP “A” Kiingilio kitakuwa ni Sh 15,000 wakati VIP “B” na VIP “C” kiingilio kitakuwa ni Sh 10,000. Viingilio hivyo vimelenga kuwaalika Watanzania wengine kwenda uwanjani.
Rais Magufuli Aagiza Nay wa Mitego Aachiwe Huru
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe, amedai kuwa Rais Dkt John Magufuli ameagiza kuachiwa huru kwa Nay wa Mitego
Dkt Mwakyembe aaedai kuwa Rais amemuambia amuelezee Nay auboreshe zaidi wimbo huo kwakuwa umegusa masuala muhimu.
Dkt Mwakyembe aaedai kuwa Rais amemuambia amuelezee Nay auboreshe zaidi wimbo huo kwakuwa umegusa masuala muhimu.
“Yaani asiondoe kitu chochote, ila aongeze kwasababu unaelezea changamoto zilizopo kwenye jamii halafu wanaitikia watu ‘wapoo’” amesema Dkt Mwakyembe kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma leo.
“Rais amesema [Nay] amesahau vitu vingine vingi, wakwepaji kodi, aongeze mambo kama hayo, wabwia unga na mihadarati wapo, wafanyabiashara wa madawa ya kulevya wapo, watanzania wanaopenda tangu asubuhi hadi jioni wao ni kwenye vijiwe tu hakuna kufanya kazi wavivu waitikie tena wapoo. Kwahiyo anasema itatusaidia sana maana ni muziki mzuri na BASATA walikuwa wameshafanya mpaka uamuzi usipigwe kokote pale, wao siwalaumu walitekeleza wajibu wao, ila leo tu nimetoka kuwaomba kipindi ambacho mimi naongoza hii wizara naomba wafanye consultation zaidi kabla ya kuchukua hatua ili katibu mkuu ajue, naibu waziri ajue tunaweza kubadilishana mawazo sababu haya mambo yanahusu haki za msingi ambazo zipo kwenye katiba ya jamhuri ya muungano,” amesisitiza Dkt Mwakyembe.
“Kwahiyo nimechukua hatua kama waziri mwenye dhamana kuwaagiza polisi wamwachie yule kijana, hebu waache kumhoji huyu kijana, badala ya kujitetea mimi ningemshauri hata aje Dodoma naweza kumuona kesho, nimwelekeze vizuri hata namna ya kuongeza wimbo utakuwa mzuri kweli kweli. Na mimi mwenyewe nimeisikiliza hii beat nakubaliana na mheshimiwa rais, rais najua anapenda muziki, lakini hata mimi mwenyewe napenda muziki kwakweli ile beat ni kali.”
Nay alikuwa tayari akichukuliwa maelezo na polisi jijini Dar es Salaam. Kwa uamuzi wa Rais Magufuli hiyo ina maana kuwa hana tena shtaka lolote la kujibu.
Diamond Aringishia Cheni na Pete zake Mpya za Shilingi Milioni 158
Pete na cheni mpya za Diamond Platnumz alizozivaa kwa wakati mmoja zina thamani ya shilingi milioni 158!
Hitmaker huyo wa Marry You amepost Instagram picha mbili zikionesha madini hayo kwa kile anachosema kuwainspire mashabiki wake.
“Thanks God for my new GOLD & DIAMONDS collection…i never thought i would be able to hang 50,000$ on my neck,” ameandika kwenye picha ya kwanza.
Kwenye picha nyingine ameandika, “Thanks God for your daily blessings never thought i would be able to walk with 22,000 $ on my Hand!!!… jus get inspired @sallam_sk don’t hate.”
Muimbaji huyo wikiendi iliyopita alitumbuiza show ya nguvu humo Muscat, Oman
Nay wa Mitego Ahamishiwa 'Central Police Station' Dar
Rapper Nay wa Mitego amehamishiwa katika kituo cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam kutoka Mvomero, Morogoro alikokuwa ameshikiliwa na polisi kuanzia asubuhi ya Jumapili, March 26.
Taarifa hiyo imetolewa na mwanasheria maaarufu nchini, Peter Kibatala.
Sunday, March 26, 2017
Mr.Nay Akamatwa na Polisi Morogoro
Kutoka Morogoro alikokuwa ameenda kwaajili ya show asubuhi
hii amethibitisha kukamatwa na Polisi,
Msanii huyo wa
Bongofleva Nay wa Mitego ambaye hivi karibuni hajasema sababu
ya kukamatwa kwake lakini watu wanahisi ni kutokana na wimbo
mpya anaodai amezungumza ukweli wa moyo wake kwa kinachoendelea,Wimbo
huo uitwao 'Wapo' umemkosoa vikali Rais Dkt John Magufuli.
Nay ameandika kwenye Instagram yake “Nimekamatwa
kweli muda huu nikiwa Hoteli Morogoro baada ya kumaliza kazi yangu iliyonileta,
napelekwa Movemero Police, Nawapenda Watanzania wote #truth #Wapo”
Mbwana Samatta Aipatia Taifa Stars Ushindi wa Mabao 2-0
Mbwana Samatta amefanya kile ambacho watanzania wengi walikuwa wanatarajia akifanye, magoli mawili aliyofunga yameipa Stars ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa ya kalenda ya FIFA iliyochezwa kwenye uwanja wa taifa.
Samatta alianza kuweka kambani dakika ya pili tu tangu kuanza kwa kipindi cha kwanza baada ya kutoka na mpira nje ya box na kuwakusanya mabeki wa Botswana na kuingia nao kwenye box kisha kumtungua kwa mguu wa kushoto golikipa wa Botswana ambaye aliruka bila mafanikio.
Samatta alianza kuweka kambani dakika ya pili tu tangu kuanza kwa kipindi cha kwanza baada ya kutoka na mpira nje ya box na kuwakusanya mabeki wa Botswana na kuingia nao kwenye box kisha kumtungua kwa mguu wa kushoto golikipa wa Botswana ambaye aliruka bila mafanikio.
Bao hilo lilidumu kwa dakika zote zilizobaki za kipindi cha kwanza huku mchezo ukiwa umechangamka kwa timu zote kushambuliana kwa zamu.
Kipindi cha pili Botswana waliamua kuliandama goli la Stars kwa mashambulizi ya mara kwa mara kwenye goli la Stars na mara kadhaa walipoteza nafasi za kufunga.
Dakika ya 87 kipindi cha pili, Samatta alifunga goli la pili na la ushindi kwa Stars kwa mkwaju wa free-kick nje kidogo ya box la penati baada ya yeye mwenyewe (Samatta) kuangushwa nje kidogo ya eneo la penati box.
Licha ya kufunga magoli mawili, Samatta aliwa kwenye wakati mgumu kwa sababu mara nyingi alikuwa akichezewa rafu zilizosababisha wachezaji wa Botswana kuoneshwa kadi za njano. Samatta ilibidi atibiwe na daktari wa Stars baada ya kufanyiwa rafu wakati akijaribu kumtoka moja ya mabeki wa Botswana.
Umahiri wa golikipa wa Botswana Kabelo Dambe umeisaidia timu yake kupunguza idadi ya magoli kutokana na kuokoa michomo ya miwili ya Mbwana Samatta pamoja na Simon Msuva.
Taifa Stars itacheza tena mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi siku ya Jumanne March 28, 2017 kwenye uwanja wa taifa
WE RISE BY UPLIFTING OTHERS
When we learn to connect with nature and people around us, we tend to uplift our potentials. The reason to this is because we tend to push people up and as they grow and become successful, we get repaid with at least the same price.
Be grateful to anyone who is in your life, they were meant for something. The purpose been either to be pulled up towards success or to stretch others to see their potentials. We can call this Mutual Success.
To help you to be the best bridge to others and to yourself, click on the video below and you will be amused;
source; JOEL OSTEEN AUDIO PODCAST
special gratitude; Kweka Yotham
Thank You!
Be Blessed!
Saturday, March 25, 2017
Stan Bakora na Kitale Ufufuo na Uzima Ministries Kwa Askofu Gwajima
Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Ministries, Josephat Gwajima amesema Jumapili hii atatembelewa na wachekeshaji Kitale ‘Mkudesimba’ pamoja na Stan Bakora.
Gwajima amekuwa akitamka mara kadhaa kwamba anavutiwa na wachekeshaji hao ambao wamekuwa maarufu kutokana na vichesho vyao ambavyo vilikuwa vinarushwa kupitia redio ya EFM.
Jumamosi hii mchungaji huyo ambaye amekuwa akizuru katika vituo mbalimbali vya redio kutoa pole kuhusiana na tukio la RC Makonda kuvamia kituo cha Clouds Media siku chache zilizopita, ametoa taarifa ya kutembelewa kanisani kwake na wachekeshaji hao.
“Tutakuwa na ugeni wa waigizaji na wachekeshaji wawili rafiki yangu Mkude Simba (Kitale) na Stan Bakora watapata nafasi ya kuperform live pia, kwa niaba ya familia ya Ufufuo na Uzima tunawakaribisha. Ufufuo na uzima tunasapoti vipawa mbalimbali ambavyo watu wamepewa na Mungu,” aliandika Gwajima Instagram.
Askofu huyo amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii hivi karibuni baada ya kutajwa kwenye sakata la dawa za kulevya na RC Makonda.
Mbwana Samatta Anamiliki Mijengo Sita Dar
Achana na uwezo wa Mbwana Samatta akiwa uwanjani. Mchezaji huyo siyo wa mchezo pia kiuchumi– ana mijengo takribani sita jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti, mshambuliaji huyo wa Taifa Stars na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji amewekeza zaidi katika kujenga nyumba ambazo zote hizo zipo Mbagala lakini katika maeneo tofauti tofauti.
Imedaiwa kuwa mijengo hiyo ya Samatta ipo Majimatitu, Kiburugwa Shimo la Mchanga, Mbande na Mbagala Saku (zote zipo Mbagala) ukiachana na ile ikulu yake anayoijenga huko kibada ambayo tayari imeisha japo kuna marekebisho madogo madogo yanaendelea.
Wakati huo huo rafiki wa karibu wa mchezaji huyo aliliambia gazeti hilo kuwa mchechezaji huyo anaishi katika nyumba yake aliyopanga (Apartment) iliyopo katika ufukwe wa bahari ya Hindi maeneo ya Kijichi.
“Anapokuja kwa mapumziko kwao huwa anakwenda kwa sababu ni nyumbani kwa ajili ya kusalimia na mambo mengine lakini hakai hapo, anaishi Kijichi kuna nyumba nzuri ya kifahari ipo ufukweni mwa bahari amepanga,”alisema.
Timu ya Serengeti Boys Yapata Chanjo
Timu ya Tanzania ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys Machi 24, wamefanyiwa chanjo ya ugonjwa wa manjano (yellow fever) kabla ya kuanza safari ya kwenda Morocco, Cameroon na Gabon.
Timu hiyo imefuzu kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Fainali hizo zinatarajiwa kuanza Mei 14 mwaka huu na mapema mwezi ujao itasafiri kwenda Morocco kwa ajili ya kambi.
Kambi hiyo itakuwa ni ya mwezi mmoja (Aprili 5 hadi Mei 1, 2017) kabla ya kuwa na kambi ya wiki moja huko Cameroon (Mei mosi hadi Mei 7, mwaka huu) na baadaye itafanya kambi nyingine Gabon (Mei 7 mpaka Mei 13) angalau kwa wiki moja kabla ya kuanza fainali hizo Mei 14, mwaka huu.
Diamond akusanya kijiji kwenye show ya Muscat
Usiku wa Ijumaa hii Diamond alifanya show kubwa ambayo ilihudhuriwa na umati mkubwa wa watu waliojitokeza kutoka sehemu mbalimbali katika mji wa Muscat nchini Oman. Hizi ni baadhi ya picha za show hiyo.
Polisi waanza kumsaka aliyemtolea bastola Mheshimiwa Nape
Jeshi la Polisi limesema limeanza kufanyia kazi maagizo waliyopatiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, kumsaka mtu aliyemtolea bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
Hayo yalisemwa Ijumaa hii na Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso. Awali, Gazeti la Mwananchi lilimtafuta Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu, lakini simu yake ilipokelewa na msaidizi wake aliyemtaka mwandishi amtafute Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ili atoe ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa agizo la Waziri Nchemba.
Alipopigiwa simu, Senso alijibu kwa ufupi kuwa wameanza kufanyia kazi agizo la Waziri Nchemba. “Sisi tumepokea maelezo ya waziri na tayari tumeanza kuyafanyia kazi, hilo ndilo ninaloweza kukwambia,” alisema.
Hali hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya polisi aliyevalia kiraia kumtishia bastola, Nape ambaye pia ni Mbunge wa Mtama (CCM). Sambamba na hayo Waziri Nchemba alilaani kitendo hicho na kumuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi kuchukua hatua.
Friday, March 24, 2017
Rais Magufuli Baada Ya Kufanya Ziara Ya Kushitukiza Bandari DSM Amekuta Haya
Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli alhamisi ya March 23 2017 amefanya ziara ya kushitukiza katika bandari ya Dar es Salaam, Rais amefanya ziara hiyo akiwa na lengo la kuthibitisha kama maagizo yake ya kusimamia na kudhibiti udanganyifu wa mizigo inayoingia.
Katika ziara hiyo Rais Magufuli ameshuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini kutoka kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa ambayo yamezuiliwa kusafirishwa nje ya nchi tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya March 2 2017.
Hata hivyo Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP – Ernest Mangu na vyombo vingine vya usalama kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo mpaka hapo uchunguzi wa utakapofanyika kubaini ukweli.
Pamoja na hayo Rais Magufuli ameona udanganyifu wa baadhi ya wafanyabiashara ambao wameingiza makontena huku nyaraka zikiandika kuwa yamebeba mitumba lakini yalipofunguliwa yalionekana yamebeba magari ya kifahari.
“Nataka niwaambie nchi yetu inachezewa mno, nimekuja kuyaona haya makontena kama yapo na kweli nimeyaona, sasa utaratibu utakapokamilika nataka Watanzania na dunia nzima ione kilichomo ndani kama ni mchanga kweli ama dhahabu” ~Rais Magufuli.
Uteuzi Mengine Wa Rais Magufuli Baada Ya Uteuzi Wa Dr. Mwakyembe na Prof. Palamagamba
Asubuhi ya March 23 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli alifanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri kwa kumteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Dr Harrison Mwakyembe kuwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Huku akimteua Prof Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, baada ya uteuzi huo Rais Magufuli jioni ya leo March 23 2017 amefanya uteuzi mwingine tena kwa mteua Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu Ikulu.
Huku akimteua Prof Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, baada ya uteuzi huo Rais Magufuli jioni ya leo March 23 2017 amefanya uteuzi mwingine tena kwa mteua Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu Ikulu.
Young Killer- Sinaga Swagger Remix Video
Mwimbaji wa bongo fleva Young Killer msodoki ametusogezea video mpya ya wimbo wake wa Sinaga Swagger remix imefanywa na director mtanzania Nicklass, ukimaliza kuitazama naomba uache na comment yako ili Msodoki akipita ajue watu wake wamempokeaje
Alichokizungumza Nape Nnauye alipokutana na Waandishi Wa Habari FULL VIDEO
Leo asubuhi ya March 23 2017 taarifa kutoka IKULU ilieleza kwamba nafasi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amepewa Dr. Harrison
Mwakyembe, baadaye Nape Nnauye alitoa taarifa kuwa atazungumza na Waandishi wa Habari lakini Meneja wa Hotel ambayo mkutano ulitakiwa ufanyike alisema ameagizwa kuwaambia Waandishi watawanyike na hakutakuwa na mkutano.
Saa chache baadae Nape Nnauye alifika eneo hilo na aliongea na waandishi akiwa juu ya gari. Bonyeza play hapa chini kutazama full video ya alichokiongea.
Mwakyembe, baadaye Nape Nnauye alitoa taarifa kuwa atazungumza na Waandishi wa Habari lakini Meneja wa Hotel ambayo mkutano ulitakiwa ufanyike alisema ameagizwa kuwaambia Waandishi watawanyike na hakutakuwa na mkutano.
Saa chache baadae Nape Nnauye alifika eneo hilo na aliongea na waandishi akiwa juu ya gari. Bonyeza play hapa chini kutazama full video ya alichokiongea.
Wednesday, March 22, 2017
Cristiano Ronaldo Ameshinda Tuzo Yake ya 11 2016/2017
Staa wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Ureno akiwashinda Pepe huku Renato Sanchez akishinda tuzo ya mchezaji bora mwenye umri chini ya miaka 21
Ronaldo ametangazwa mshindi wa tuzo hiyo huku kocha wao wa timu ya taifa ya Ureno aliyowaongoza kushinda michuano ya Euro 2016 Fernando Santos kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka. Hii ni tuzo ya 11 ya Ronaldo toka 2016/2017 baada ya tuzo ya mchezaji bora wa Dunia wa FIFA aliyoichukua January 9 2017.
Site Users
Popular Posts
Topics
News
(108)
Artists
(83)
Local
(45)
Views
(41)
Music
(38)
International
(36)
Relationships
(34)
Universities
(28)
Sports
(25)
Sports Stars
(25)
Business
(14)
Life Style
(14)
Actors
(10)
OFFclass
(10)
Entrepreneur
(9)
Events
(9)
Health
(9)
Hustles
(9)
Who Hit A Lottery?
(7)
Fashion
(4)
High Schools
(4)
Movies/TV Series
(4)
Talent
(3)
Education
(1)
Tech
(1)
Archive
-
▼
2017
(182)
- November 2017 (2)
- September 2017 (20)
- August 2017 (46)
- July 2017 (6)
- June 2017 (2)
- May 2017 (1)
- April 2017 (45)
- March 2017 (51)
- February 2017 (8)
- January 2017 (1)
-
►
2016
(94)
- December 2016 (1)
- November 2016 (3)
- October 2016 (22)
- September 2016 (68)